SUDANI KUSINI-SALVA KIIR-RIEK MACHAR

Mapigano makali Juba

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na Makamu wake wa kwanza Riek Machar, katika Ikulu ya mjini Juba, Aprili 26, 2016.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na Makamu wake wa kwanza Riek Machar, katika Ikulu ya mjini Juba, Aprili 26, 2016. REUTERS/Stringer

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa Jumatatu hii katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na vile vinavyomuunga mkono Makamu wa kwanza wa rais, Riek Machar.

Matangazo ya kibiashara

Ndege za kivita na vifaru vimeonekana vikitumiwa katika mapigano hayo. Hali hii imesababisha usalama kudoroa katika taifa hili changa duniani, na kutishia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hayo yakijiri Serikali ya Marekani, imetaka kusitishwa mara moja kwa vurugu nchini Sudan Kusini, baada ya kutokea mapigano mapya, jijini Juba, mapigano yanayotishia kuvunjika kwa mkataba wa amani kwenye taifa hilo jipya kabisa duniani.

Mapigano haya ni ya kwanza kati ya jeshi la Serikali na wanajeshi waasi mjini Juba, toka kurejea nyumbani kwa kiongozi wao, Riek Machar mwezi April mwaka huu, na kuchukua nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais, kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu nchini humo kwa miaka 3.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imeagiza kuondoka nchini humo kwa raia na wafanyakazi wake, na kulaani taarifa kuwa raia wa kawaida wemeshambuliwa, ambapo mpaka sasa watu 150 wamekufa kutoka kila upande.

"Natoa wito kwa utulivu na kujizuia katika mapigano hayo. Mimi niko salama Hakuna anayeweza kutumia haki yake kwa kuhatarisha usalama wa nchi, " Riek Machar ameandika kwenye akautnti yake ya Twitter.

Inaarifiwa kuwa askari wasiopungua watano waliuawa Alhamisi iliyopita na, kwa mujibu wa chanzo cha Wizara ya Afya ya Sudan Kusini, watu 272, wakiwemo raia 33,

Watu walioyahama makazi yao katika mji wa Juba, Sudan Kusini.
Watu walioyahama makazi yao katika mji wa Juba, Sudan Kusini. REUTERS/James Akena

waliuawa siku ya Ijumaa pekee.