AFRIKA KUSINI-UFARANSA

Ziara ya Zuma Ufaransa: Mikataba sita ya ushirikiano yasainiwa

Le président sud-africain, Jacob Zuma, a été reçu par son homologue français, François Hollande, à Paris, le 11 juillet 2016.
Le président sud-africain, Jacob Zuma, a été reçu par son homologue français, François Hollande, à Paris, le 11 juillet 2016. REUTERS/Jeremy Lempin/Pool

Bendera za Afrika Kusini zimekua zikipepea kwenye Ikulu ya Champs-Elysées katikati mwa mji wa Paris kwa heshima ya Jacob Zuma, katika ziara ya kikazi ya siku mbili. Rais wa Afrika Kusini amepokelewa na François Hollande Jumatatu hii asubuhi Julai 11 na katika tukio hili, mikataba sita ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili imesainiwa.

Matangazo ya kibiashara

Mikataba hiyo sita ya ushirikiano iliafikiwa katika nyanja za nishati, utamaduni, elimu na hali ya hewa. Baada ya zaidi ya saa moja ya mazungumzo, wakuu hao wa nchi wametangaza ikiwa ni pamoja na Mkataba wa ufadhili wa Euro milioni 60 kwa ajili ya maendeleo ya nishati mbadala na makubaliano juu ya ufuatiliaji wa uvuvi katika eneo la kusini.

Jacob Zuma ameongozana na mawaziri wanane na viongozi mia moja wa makampuni, ambao walishiriki asubuhi katika jukwaa la biashara katika makao makuu ya Medef. Hata hivyo, hakuna mkataba wowote ule wa kibiashara uliyotangazwa.

Mshirika wa kwanza wa uchumi wa Ufaransa barani Afrika

Viongozi hao wawili wamehakikisha kwamba kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya hautoathiri uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Badala yake, Rais wa Ufaransa, François Hollande, amesisitiza kuwa ziara hii kwa kiasi kikubwa itaimarisha ushirikiano kati ya Afrika Kusini na Ufaransa, kisiasa na kiuchumi.

"Tuna ushirikiano wa kisiasa ambao tumeamua kuongeza zaidi. Na sisi, kama vile, juu ya utandawazi katika toleo lake la kiuchumi kama katika toleo lake la kimazingira, kunaweza kuwa na maendeleo. Katika suala hili, tumesaini mkataba ambao utaruhusu Taasisi ya Maendeleo ya Ufaransa kutekeleza, pamoja na makampuni ya Afrika Kusini, miradi ya nishati mbadala na ufanisi wa nishati, " Rais wa Ufaransa François Hollande, amesema.