SUDANI KUSINI-BAN-UN

Machafuko Sudan Kusini: Ban Ki-moon atoa wito kwa hatua kali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuichukulia vikwazo vya silaha Sudan Kusini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuichukulia vikwazo vya silaha Sudan Kusini. ©REUTERS/Heinz-Peter Bader

Baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani vurugu nchini Sudan Kusini na wito kwa Rais Salva Kiir na Makamu wa Rais Riek Machar kurejesha utulivu nchini, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amewaonya Jumatatu wiki hii viongozi wa Sudan Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mbele ya waandishi wa habari, ameelezea kuchanganyikiwa kwake katika hotuba dhidi ya Baraza la Usalama akibaini kwamba inapuuzia baadhi ya mambo akiitaka kuchukua hatua haraka iwezekanavyo.

Jumatatu wiki hii, Ban Ki-moon ametolea maneno kali dhidi ya viongozi wa Sudan Kusini na viongozi wa kijeshi. "Kwa mara nyingine tena, viongozi wa Sudan Kusini wamewasaliti raia wao. Viongozi wa Sudan Kusini, mpaka sasa, hawajatimizi hawajatimiza ahadi zao, kwa hiyo wanatakiwa kuzitimiza haraka iwezekanavyo, ametangaza. Ni aina gani ya uongozi tutakabiliana nao wakati unatumia silaha na siasa ya aina moja, miaka yote hiyo? Uongozi unaosaliti raia wake. Ujumbe wangu kwa Rais Salva Kiir na Makamu wa Rais Riek Machar uko wazi: Fanyeni kila kilio chini ya uwezo wenuna ili machafuko yakome mara moja. Tuone maagizo kwa vikosi vyenu husika kurudi katika makambi yao. Napenda kusisitiza tena, kwa wale wanaofanya mashambulizi haya kama vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa dhidi ya raia, Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa mashirika ya kiutu yanaweza kuwa uhalifu wa kivita. Lazima sheria ifuate mkondo wake kwa watu waliohusika na vitendo viovu nchini Sudan Kusini tangu mwaka 2013. "

"Ni wakati wa kuimarisha kwa wingi kazi ya Umoja wa Mataifa. Wakati serikali haiwezi au haitaki kulinda raia wake, au wakati pande husika madarakani zinataka kupata utajirikwenye migongo ya raia wake, jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuchukua hatua, " Ban Ki-moon amesema.

Vikwazo vya silaha na vikwazo kwa watu wanaochochea machafuko

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua maamuzi matatu: kupigia kura vikwazo vya silaha, vikwazo dhidi ya dhidi ya viongozi wanaohusika na machafuko dhidi ya raia wa Sudan Kusini na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Na hatimaye kuzishawishi nchi wanachama kutuma helikopta za kivita ili kuruhusu Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), kutimiza wajibu wake.