SUDANI KUSINI-SALVA KIIR-RIEK MACHAR

Sudan Kusini: hali ya utulivu yarejea baada ya siku kadhaa za vurugu

Nchini Sudan Kusini, hali ya utulivu imerejea baada ya siku nne za mapigano makubwa katika mji mkuu Juba. Jumatatu usiku, usitishwaji wa mapigano ulisainiwa na Rais Salva Kiir na Riek Machar, wakati ambapo Ban Ki-moon alitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuimarisha kijeshi tume yake nchini Sudan Kusini na kuchukua vikwazo vya silaha.

Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, tarehe 12 Julai 2016, ukiwa tupu baada ya mapigano mwishoni mwa wiki hii.
Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, tarehe 12 Julai 2016, ukiwa tupu baada ya mapigano mwishoni mwa wiki hii. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Saa 24 baada ya usitishwaji mapigano uliosainiwa na pande zote mbili, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa watu 36 000 katika mji wa Juba wamelazimika kuyahama makazi yao kwa sababu ya mapigano.

IGAD, Mamlaka ya Maendeleo katika Ukanda wa Afrika Mashariki, imetoa wito kwa ufunguzi wa barabara kwa minajili ya kusafirisha misaada ya kibinadamu. Na kwa sababu hiyo vizuizi barabarani vimezorotesha shughuli za vikosi vya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali, amesema mwanadiplomasia wa jumuiya inayoundwa na nchi nane za Afrika ya Mashariki.

UNMISS yakosolewa

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imekua ikinyooshewa kidole kwa kutochukua hatua mwishoni mwa wiki iliyopita. Ban Ki-moon, Jumatatu wiki hii, ametoa wito wa kuimarisha kikosi cha Umoja wa Mataifa, wakati ambapo katika kambi ya Riek Machar, wanaomba vikosi vya Umoja wa Mataifa kujihusisha zaidi na hali inayojiri Sudan Kusini. "Kama UNMISS, inaweza eneo huru, hivyo labda usitishwaji wa mapigano utadumu," amesema James Gatdek Dak msemaji wa SPLA / IO (SLPA / In Opposition) kundi linalomuunga mkono Makamu wa rais Riek Machar.

Idadi ya watu walipoteza maisha katika mapigano hayo ya siku nne bado haijajulikana. Lakini vyanzo vya ndani vinabaini kwamba kwa sasa karibu watu 300 waliuawa. Lakini ni takwimu ambayo inatarajiwa kuangaliwa upya, kwani idadi hii ni ya siku ya Ijumaa pekee.

Wanajeshi wa Serikali na waasi wa zamani waliokua wakipambana hadi sasa wanaonekana kuwa wameingia katika makambi, na maduka yameanza kufungua hatua kwa hatua katika baadhi ya maeneo ya mji.