Habari RFI-Ki

Tanzania kudhibiti vituo vya tiba mbadala na tiba asilia

Sauti 10:31
Naibu waziri wa Afya nchini Tanzania, Dr Hamis Kigwangalla
Naibu waziri wa Afya nchini Tanzania, Dr Hamis Kigwangalla Bunge la Tanzania

Serikali nchini Tanzania imefuta usajili wa baadhi ya Vituo vya tiba asilia,na vingine kusitisha huduma zao kutokana na kukiuka masharti ikiwemo urushaji wa matangazo yasiyokuwa na kibali kutoka katika baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala pamoja na baadhi ya waganga kuendelea kutoa elimu ya tiba asili na tiba mbadala kwa umma kinyume cha katazo la wizara ya afya.hivi karibuni kumekuwepo na baadhi ya matangazo na vipindi vinavyorushwa katika redio, magazeti, runinga na mitandao ya kijamii kuhusu utoaji wa matibabu ya tiba asili na tiba mbadala kinyume cha utaratibu na maadili.