COTE D'IVOIRE-GRAND BASSAM-MAUAJI

Askari wa Cote d'Ivoire wafuatiliwa kuhusu shambulio la Grand-Bassam

Askari wa Côte d’Ivoire katika mji wa Grand-Bassam, Machi 13, 2016, siku ya shambulio.
Askari wa Côte d’Ivoire katika mji wa Grand-Bassam, Machi 13, 2016, siku ya shambulio. © REUTERS/Luc Gnago

Kwa mara ya kwanza, askari watuhumiwa katika sehemu ya uchunguzi kuhusu shambulio la Grand-Bassam. Taarifa hii imetolewa Jumatano hii na mwendesha mashitaka wa kijeshi. Askari wawili wanashtakiwa kwa "ukiukaji wa mafundisho ya kijeshi."

Matangazo ya kibiashara

Wanatuhumiwa kuwa walikua na taarifa kuhusu nia ya wanajihadi na kwamba hawakutoa taarifa hiyo. Machi 13, shambulizi la kigaidi katika katikaeneo la pwani la mji wa Grand-Bassam, mji mdogo uliokaribu na bahari karibu na mji mkuu wa Cote d'Ivoire, Abidjan, lilisababisha vifo vya watu 19. Kwa mujibu wa Serikali ya Cote d'Ivoire, zaidi ya watu 80 walikamatwa katika nchini humo katika uchunguzi wa shambulio hilo.

askari wawili waliokamatwa kwa muda mrefu waliishi katika katika kata hiyo ya Abidjan kama magaidi wa shambulio hilo la Grand-Bassam. Mara kadhaa, kwa mujibu wa mwendesha mashitaka wa kijeshi, askari hao walikua wakizungumza na magaidi na hasa na dereva wao. Vifaa muhimu vya kigaidi vilikamatwa mwezi Juni katika mji mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire.

Askari hao wawili watuhumiwa kuwa na taarifa ya nia ya magaidi lakini hawakutoa taarifa hiyo. Mashtaka ambayo hakuna hata mmoja kati ya askari hao anayoyatambua, amesema mwendesha mashitaka wa kijeshi. "Wanatuambia kwamba hawakujua kwamba walikuwa wanajihadi. Tumewajibu kwamba, "wangelipaswa kujua, " amesema Ange Kessi.

Katika hatua hii, hata hivyo, hawajakbiliwa na kosa. Hakuna dalili zinazoonyesha kwamba waliwasaidia magaidi, amesema mwendesha mashitaka, lakini uchunguzi unaendelea. watu wawili, mmoja akiwa askari katika kikosi cha ulinzi cha wa Rais, na mwengine ni askari katika bataliani ya San Pedro, magharibi mwa nchi, watahukumiwa mwishoni mwa mwezi Agosti. Zaidi ya watu 80 walikamatwa kuhusiana na uchunguzi wa shambulizi la Grand-Bassam.