SUDANI KUSINI-MAREKANI

Sudan Kusini: Marekani yatuma askari wa kulinda ubalozi wake

Wanajeshi wa Marekani watumwa Sudan Kusini.
Wanajeshi wa Marekani watumwa Sudan Kusini. REUTERS/Omar Sobhani/File Photo

Marekani iimetuma askari 47 nchini Sudan Kusini. Askari hao waliwasili Jumanne juu katika mji wa Juba, na kazi yao ni kulinda raia wa Marekani, ubalozi na mali ya Marekani, wakati ambapo nchinyingi zimekua zikiwarejesha nyumbani raia wao.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajadili uwezekano wa kuongeza muda wa kikosi chake nchini humo (UNMISS), pamoja na uwezekano wa kuimarisha vikwazo vya silaha.

Toka siku ya Jumapili, wafanyakazi wasio muhimu kwenye ubalozi wa Marekani walirejeshwa nyumbani, na wale walio salia nchini Sudan Kusini walipewa maelekezo ya tahadhari.

Katika barua Barack Obama alitumia Baraza la wawakilishi katika ahadi yaeke ya kutuma kikosi cha askari hao nchini Sudan Kusini, alisema kuwa askari hao 47, licha ya kuwa na silaha nzito nzito za kivita, hawaruhusiwi kupigana.

Rais wa Marekani ameongeza kuwa askari 130 wa ziada walioko nchini Djibouti, wako katika hali ya tahadhari na wako tayari kuingilia kati ikiwa hali itazidi kuzorota zaidi nchini Sudan Kusini.

Aidha, katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje, Washington imerejelea kulaani vurugu ambazo zilisababisha maelfu ya raia kuyahama makazi yao, na kusema kuwa wale waliohusika katika ukiukwaji wa haki za binadamu na mashambulizi dhidi bikosi vya Umoja wa Mataifa, watafuatiliwa na vyombo vya sheria.