Amnesty: “Mazingira wanakofungwa wapiganaji wa Boko Haram ni mabaya”

Picha iliyonaswa katika video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, Januari 20 2015.
Picha iliyonaswa katika video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, Januari 20 2015. © AFP PHOTO / BOKO HARAM

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International linasema idadi kubwa ya watuhumiwa wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa katika mazingira mabaya katika magereza mbalimbali nchini Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Shirika hilo imesema kuwa wengi wa wafungwa hao wamepoteza maisha kwa sababu ya maradhi mbalimbali, wengine wakiteswa na hata kunyimwa chakula.

Amnesty International inasema serikali ya Cameroon imewazuaia zaidi ya washukiwa 1000 wa Boko Haram bila ya kuwafikisha Mahakamani, kuwafungulia mashtaka ya ugaidi.

Cameroon ni mojawapo ya nchi za Afrika Magharibi inayokabiliana na kundi hilo ambalo ambalo limesababisha vifo vya maelfu ya watu Kaskazini mwa Nigeria.

Hivi karibini ilitangazwa kuwa kiongozi wa kundi hilo huenda aliuawa katika mashambulizi ya jeshi la Nigeria, lakini siku chache baada Abubakar Shekau alionekana katika video iliyorushwa hewani katika mitandao ya kundi la Boko Haram akisema kuwa bado hajafa, na atakufa kwa amri ya Mungu wala sio ya binadamu.

Boko Haram imesababisha vifo vya watu wengi katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi.