AU-UCHAGUZI

Uchaguzi wa Mwenyekiti wa AU kutofanyika juma hili

Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika. REUTERS/Tiksa Negeri

Uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika huenda usifanyike wiki hii, baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa mataifa yenye usemi mkubwa yanataka zoezi hilo kuahirishwa hadi pale wagombea wenye hadhi ya juu watakapopatikana.

Matangazo ya kibiashara

Duru zinasema kuwa wagombea wote walioomba kuchaguliwa wanaonekana kuwa hawana vigezo kuchukua nafasi hii ambayo kwa sasa inashikiliwa na Dr Nkosazana Dlamini Zuma ambaye alitangaza kujiuzulu.

Mataifa yanayotaka uchaguzi huo kuahirishwa hadi Januari mwaka ujao ni yale ya Afrika Magharibu huku yale ya Kusini mwa Afrika yakisema hayajakubaliana mgombea wa kumuunga mkono.

Hata hivyo, Mataifa ya Afrika Mashariki yameamua kumuunga mkono aliyekuwa Makamu wa rais wa Uganda Bi Specioza Kazibwe.

Mgombea mwingine ni Waziri wa Mambo ya nje wa Boswtana Bi Pelonomi Venson- Moitoi.