Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Viongozi wa AU kujadili Sudan Kusini leo

Imechapishwa:

Mtazamo wako kwa yaliyojiri juma hili imeangazia mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa mjini Nice ambapo gaidi aliendesha lori lake kuelekea umati wa watu  wakati wakisherehekea siku ya kitaifa ya mapinduzi, huku kukirushwa fataki Alhamisi usiku.Tumeangazia pia mkutano wa viongozi wa mataifa ya Umoja wa Afrika AU, leo mjini Kigali nchini Rwanda, kujadili juu ya mgogoro wa Sudan Kusini, na huko DRC Mkuu wa tume ya Umoja wa mataifa Monusco kuelezea kuridhika kwake na maandalizi ya mjadili wa kitaifa unaotazamiwa kufanyika Kinshasa mwishoni mwa mwezi huu wa Julai 2016. 

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika UA, Nkosazana Dlamini-Zuma, pembeni yake ni Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, January 29 2016 mjini Addis-Abeba.
Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika UA, Nkosazana Dlamini-Zuma, pembeni yake ni Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, January 29 2016 mjini Addis-Abeba. TONY KARUMBA / AFP
Vipindi vingine