KIGALI-UMOJA WA AFRIKA

Mapigano ya Juba kutawala mkutano wa Umoja wa Afrika Kigali

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban-Ki-moon akisalimiana na raisi Salva Kiir mjini Juba 25 februari 2016.  i
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban-Ki-moon akisalimiana na raisi Salva Kiir mjini Juba 25 februari 2016. i REUTERS/Jok Solomon

Mapigano mapya ya hivi karibuni nchini Sudani Kusini yaliyogharimu maisha ya takribani watu laki tatu yanatarajiwa kutawala majadiliano ya mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika unaoanza jumapili katika jiji kuu la Kigali nchini Rwanda.

Matangazo ya kibiashara

Usitishwaji wa mapigano umefanyika kuanzia jumatatu iliyopita baada ya kushuhudia mapigano ya takribani siku nne mfululizo katika jiji kuu la Sudani kusini Juba,ambapo mamia wamepoteza maisha na wengine arobaini elfu kukimbia makazi yao.

Ghasia zilizoibuka zimeamsha shaka juu ya makubaliano ya amani yaliyokwama August 2015 kati ya pande hizo mbili.

Akizungumza na wakuu wa Jumuia ya Maendeleo ya nchi za Mashariki na pembe ya Afrika IGAD jumamosi mjini Kigali,katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon alisema Sudani Kusini imefikia kiwango kibaya cha mzozo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza, rais Kiir amesema hataki tena kushuhudia umwagaji damu nchini humo na kumtaka Machar kuwa karibu naye ili kwa pamoja wakubaliane namna ya kuzuia mapigano kama haya katika siku zijazo.

Rais Kiir ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kiongozi wa waangalizi wa utekelezwaji wa mkataba wa amani rais wa zamani wa Bostwana Festus Mogae na Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika nchini humo Alpha Oumar Konare, katika Ikulu ya Juba.