MOROCCO-AU

Mfalme wa Morocco atangaza nia yake ya kurejea katika AU

Mfalme wa Morocco Mohammed VI.
Mfalme wa Morocco Mohammed VI. AFP PHOTO/FADEL SENNA

Mfalme Mohammed VI ametangaza Jumapili Julai 17 kwamba "wakati umewadi kwa Morocco kurejea " katika Umoja wa Afrika (AU). Morocco ilijiondoka katika Umoja wa Afrika mwaka 1984 kwa kupinga dhidi ya kukubaliwa kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi iliyotangazwa na kundi la wapiganaji la Polisario.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa muda mrefu marafiki zetu wanatuomba tuwarejelee, ili Morocco ipewe nafasi yake ya asili ndani ya taasisi hiyo. wakati huo umefika, " amesema mfalme wa Morocco katika ujumbe alioutuma katika mkutano wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Kigali, kwa mujibu wa shirika la habari la Morocco la MAP.

"Kupitia kitendo hiki cha kihistoria na wajibu wa kurudi, Morocco inapania kuhudumu ndani ya Umoja wa Afrika ili kukomesha mgawanyiko," Mohammed VI amesema. Amerejelea sababu ziliyopelekea Morocco kuchukua uamuzi, mwaka 1984, wa kujiondoa katika Umoja wa Afrika (OAU) - iliyotangulia Umoja wa Afrika(AU), kufuatia kukubaliwa kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi (SADR).

Uhuru wa taifa hili lililotawaliwa na Uhispania katika enzi za ukolonina kuunganishwa na Morocco, ulitangazwa na kundila wapiganaji la Polisario Front, lililoanzishwa mwaka1973. Baada ya miaka ya kadhaa ya mapambano ya silaha, mkataba wa usitishwaji wa mapigano ulitangazwa mwaka 1991. "Ilikua vigumu kuluutambua uhuru wa taifa hili kwa raia wa Morocco," amesema Mohammed VI katika ujumbe wake. Wakati huo, "uhuru huo uliyokubaliwa kwa shingo upande, licha ya kuwa ilikua mapinduzi dhidi ya uhalali wa kimataifa, ulipelekea utawala wa kifalme wa Morocco kuepuka mgawanyiko wa Afrika kwa gharama ya uamuzi unaoumiza, uamuzi wa kujiondoa katika Umoja wa Afrika" .

Kwa sasa, amesema Mfalme, "Umoja wa Afrika unapaswa kufuata sheria na kukosoa makosa yaliyofanywa awali," amesema Mohammed VI. Uamuzi wa kurudi kwa Morocco ndani Umoja wa Afrika utapitishwa kwa kura ndani ya Tume ya AU.