RWANDA-AU

Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika kuchaguliwa leo

Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika, atachaguliwa leo katika mkutano wa viongozi wa nchi wa bara hilo wanaokutana jijini Kigali nchini Rwanda.

Nkosazana Dlamini-Zuma, rais wa Tume ya Umoja wa Afrika anayemaliza muda wake
Nkosazana Dlamini-Zuma, rais wa Tume ya Umoja wa Afrika anayemaliza muda wake www.au.int
Matangazo ya kibiashara

Mshindi wa leo atachukua nafasi ya Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma anayeachia nafasi hiyo baada ya kuhudumu kwa miaka minne.

Wagombea wa nafasi hiyo ni aliyekuwa Makamu wa rais wa Uganda Specioza Wandira Kazibwe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Bostwana Pelonomi Venson-Moitoi na Agapito Mba Mokuy ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya nje ya Equatorial Guinea.

Wiki iliyopita, kulikuwa na wasiwasi ikiwa uchaguzi huu ungekuwepo wakati wa kikao hiki cha 27 kwa madai kuwa hapakuwa na mgombea sahihi wa kuchukua nafasi ya Bi.Zuma.

Viongozi wa mataifa ya Afrika wakiwa jijini Kigali nchini Rwanda
Viongozi wa mataifa ya Afrika wakiwa jijini Kigali nchini Rwanda CYRIL NDEGEYA / AFP

Majukumu makubwa ya Mwenyekiti mpya itakuwa ni kushughulikia maswala ya amani, usalama na siasa barani Afrika, biashara na viwanda, miundo mbinu, maswala ya kijamii na Sayansi na teknolojia.

Dlamini Zuma kutoka Afrika Kusini alichaguliwa katika nafasi hiyo mwaka 2012 na kuchukua nafasi ya Jean Ping kutoka Gabon.