CAR-CAMEROON-USALAMA

RCA: mateka 11 wa Cameroon waachiwa huru

Askari wa Cameroon katika kituo cha mpakani cha Garoua-Boulaï, katika mji wa mashariki mwa Cameroon, mji ulio karibu na waliko tekwa nyara mateka wa Cameroon Machi 2015.
Askari wa Cameroon katika kituo cha mpakani cha Garoua-Boulaï, katika mji wa mashariki mwa Cameroon, mji ulio karibu na waliko tekwa nyara mateka wa Cameroon Machi 2015. AFP PHOTO / REINNIER KAZE

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), mateka 11 wa Cameroon waliokua walitekwa nyara na kundi la waasi nchini Cameroon mwezi Machi mwaka 2015 wameachiwa huru. Wawili miongoni mwao walikufa kutokana na kifua kikuu.

Matangazo ya kibiashara

Wanaume hao na wanawake 11 wanaosalia walikua wakishikiliwa mateka katika eneo la Zoukombo, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati ambapo walikua wakitokea kwenye mazishi, kilomita karibu 11 km kutoka Garoua-Boulaï, mji wa mkoa wa Mashariki mwa Cameroon.

Rais wa Cameroon Paul Biya, ambaye alitoa taarifa hiyo Jumapili jioni Julai 17 katika taarifa yake: ". Mateka 11 wa Cameroon wako huru, na kwasa wako chini ya ulinzi wa mamlaka ya nchi" Jumanne hii, mateka hao wa zamani wamerejeshwa nchini Cameroon na wamepelekwa hospitalini kwa ajili ya tathmini ya hali ya afya zao.

Bado haijulikani hali halisi yakuachiliwa kwao, na kazi iliyofanywa na Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati au MINUSCA katika mazungumzo hayo. Tume ya Umoja wa Mataifa imekaribisha kuachiliwa huru kwa mateka hao na ilipata fursa ya kukumbusha "makundi yenye silaha kuachana na vita bila masharti."

Kutokua na uhakika

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati haikutaka kutoa maelezo zaidi kuhusu kuachiliwa kwa mateka hao. Nchini Cameroon, Rais wa nchi hiyo "amepongeza vikosi vya ulinzi na usalama vya Cameroon na kuwachukuru kwa dhati wale wote ambao, kutoka karibu au mbali, wamewajibika ili mateka hao waachilwe huru."