Habari RFI-Ki

Umoja wa Afrika wazindua pasi ya pamoja ya kusafiria

Sauti 10:28
Rais wa Rwanda  Paul Kagame (Kushoto), rais wa Chad Idriss Derby (Katikati) wakionesha pasi zao za Afrika baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Dkt .Nkosazana Dlamini-Zuma (Kulia)
Rais wa Rwanda Paul Kagame (Kushoto), rais wa Chad Idriss Derby (Katikati) wakionesha pasi zao za Afrika baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Dkt .Nkosazana Dlamini-Zuma (Kulia) The Insider

Umoja wa Afrika umezindua Pasi ya kusafiria ya bara Afrika, kuwawezesha Waafrika kusafiri na kufanya biashara katika mataifa yote 54 bila ya vikwazo, kuelekea kutimiza Ajenda ya mwaka 2063 ya kuliunganisha bara la Afrika kisiasa.Uzinduzi huu ulifanyika jijini Kigali nchini Rwanda katika mkutano wa viongozi wa Afrika, na watu wa kwanza kupata pasi hiyo ni rais wa Rwanda Paul Kagame na Mwenyekiti wa Umoja huo Idriss Derby ambaye pia ni rais wa Chad.AU imetoa hadi mwaka 2018 kuanza kutolewa kwa Pasi hiyo kwa waafrika wengine.