DRC-MAUAJI

Watu 7 wauawa katika mashambulizi ya FDLR na Mai Mai Nyatura

Watu saba waliuawa na wengine watano kujeruhiwa wakati wa shambulio la watu wenye silaha usiku wa Jumatatu Julai 18 katika kijiji cha Kibirizi katika wilaya ya Rutshuru, mkoani Kivu Kaskazini.

Tangu mwanzo wa mauaji mwezi Oktoba 2014 katika Wilaya ya Beni, wakazi wengi wameyahama makazi yao kwenye barabara kuu katika maeneo ya Oicha na Eringeti.
Tangu mwanzo wa mauaji mwezi Oktoba 2014 katika Wilaya ya Beni, wakazi wengi wameyahama makazi yao kwenye barabara kuu katika maeneo ya Oicha na Eringeti. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya jamii wanahusisha mshambulizi hilo waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR wakishirikiana na kundi la Mai Mai Nyatura. Lakini afisa wa serikali katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini amesema wanaendelea na uchunguzi ili kubaini wauaji.

Mtoto wa mwaka mmoja na wanawake kadhaa ni miongoni mwa wahanga, waliouawa wakikutwa ndani ya nyumba zao.

Wauaji wametekeleza uovu wao huo bila hofu yoyote kwa muda wa masaa mawili, wakiingia nyumba kwa nyumba, bila msaada wowote kwa raia kutoka upande wa jeshi la Congo (FARDC), wakazi wa kijiji cha Kibirizi wamelalamika.

Hali ya taharuki ilikua imetanda mapema asubuhi kati ya jamii. Makabila mengine yanaituhumu jamii ya Wahutu, ambapo wengi wao waliondoka katika kijiji cha Kibirizi Jumatatu iliyopita kwa sababu ya kukosekana kwa usalama. Watu kutoka jamii ya Wahutu wanashtumiwa pia kuandaa mashambulizi hayo kwa msaada wa kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR.

Vijana wa kijiji cha Kibirizi wenye hasira walimua mtu mooja kwa kumpiga mawe, akituhumiwa kula njama na wauaji.

Wakati huo huo, shughuli zote zimekwama Jumanne hii katika kijiji cha Kibirizi, ambapo watu wengi wameondoka kijiji hicho wakielekea katika maeneo mengine salama.

Hayo yakijiri, watu wawili wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya wanamgambo kushambuliwa lori katika kijiji cha Kyanyunda, kilomita 2 kaskazini mwa mji wa Sange, mkoani Kivu ya kusini). Mmoja watu hao alifariki papo hapo na mwengine alifariki alipofikishwa hospitalini.

Mkuu wa jeshi katika eneo la Mutarule, Bahati Kigangu, amethibitisha shambulio hilo.

Mwezi Machi, madereva wa magari ya uchukuzi walisitisha shughuli yao kwenye barabara kati ya Goma na Butembo, Bunagana, Ishasha, Vitshumbi na Kibirizi kwa sababu ya ukosefu wa usalama katika sehemu hii ya mashariki mwa DRC.