UGANDA-CAR-LRA

LRA yazidisha vitendo vyake vya utekaji nyara

Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda la LRA.
Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda la LRA. AFP

Waangalizi wa Kimataifa wanasema, utekaji nyara unaotekelezwa na kundi la waasi la Lords Resistance Army umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana kufikia katikati ya mwaka huu hasa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Hili limebainika wakati huu nchi ya Uganda ikitishia kujiondoa kwenye operesheni ya kuwasaka waasi hao wanaoongozwa na Joseph Kony.

Ripoti zinasema kuwa kundi hilo limewateka zaidi ya watu 490 kati ya mwezi Januari na mwezi Juni mwaka huu wakiwemo watoto.

Jeshi la Umoja wa Afrika likishirikiana na vikosi maalum vya Marekani, limekuwa likiendeleza Operesehni ya kumtafuta Kony ambaye hadi sasa hajakamatwa.