MALI-USALAMA

Shambulizi la Nampala: Serikali mbioni kujibu

Rais Ibrahim Boubacar Keïta akiongoza kikako cha baraza la usalama la kitaifa baada ya shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Nampala, Jumanne, Julai 19, 2016.
Rais Ibrahim Boubacar Keïta akiongoza kikako cha baraza la usalama la kitaifa baada ya shambulio dhidi ya kambi ya jeshi ya Nampala, Jumanne, Julai 19, 2016. © HABIBOU KOUYATE / AFP

Baada ya shambulizi la kambi ya jeshi ya mjini Nampala Jumanne wiki hii katikati mwa Mali, ambapo askari 17 wa Mali waliuawa, na wengine zaidi ya thelathini waliojeruhiwa, serikali imeahidi kujibu haraka shambulizi hilo na kukamilisha uchunguzi.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta amepokea Mawaziri kadhaa katika kikao cha baraza la usalama la kitaifa. Shambulizi hilo lilidaiwa rasmi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Macina Ansar Dine. Lakini saa chache kabla, kundi jipya la watu kutoka jamii ya Peul pia lilidai kuhusika na shambulio hilo.

Shambulizi lilikua kubwa na na liliratibiwa. Siku tatu kabla ya shambulizi hilo, kulishukiwa kuwepo kwa makundi ya watu wenye silaha katika eneo la Nampala. Na ndio maana Rais Ibrahim Boubacat Keita, katika kikao cha baraza la usalama la kitaifa alibaini kwamba kuna udhaifu fulani katika askari wa kambi hiyo ya Nampala.

Kulingana na taarifa zetu, washambuliaji walikata mawasiliano katika kambi ya Nampala na ngome zake muhimu.

Yote yalianza mapema Jumanne asubuhi. Watu wenye silaha za kivita walishambulia kambi kuu ya mjini Nampala kusini mwa mji wa Bamako. Hii ni kambi muhimu ya jeshi la Mali na washambuliaji, kwa mujibu wa mashahidi, walikua na magari yaliyojaa vifaa vya kijeshi.

Baada ya mapigano ya muda mrefu, walichukua udhibiti wa kambi hiyo na kupandisha bendera nyeusi. Kisha waliwasha moto na mashahidi walikua wakiona wakiwa mbali na kambi hiyo. Moshi mkubwa ulikua ukitokea katika kambi hiyo Jumanne hiii.

Kutoka kilomita 80 na mji wa Nampala, katika kijiji cha Niono, mashahidi waliona magari ya wagonjwa yakibeba askari wa Mali waliojeruhiwa.

Sidi Cissé, Rais wa muungano kwa ajili ya kuhifadhi utambulisho wa jamii ya Peul, amedai kuwa kundi lake ndio limehusika na uvamizi huo. Kundi hili lilianzishwa muda si mrefu, lakini kinachoeleweka ni kwambashirika kuu la masuala ya utamaduni ya jamii ya Peul, ya watu wa jamii ya Peul kutoka Mali, Tabital Pulaaku, amesema kuwa hawalitambui kundi hilo.