LIBYA-UFARANSA

Libya: serikali ya umoja yaishtumu Ufaransa kwa "ukiukaji" wa ardhi yake

Tangazo la vifo vya askari wa tatu wa Ufaransa waliouawa wakiwa katika shughuli ya upelelezi nchini Libya imesababisha kuibuka kwa hisia mbalimbali nchini humo. Bunge la Mashariki limesema kusikitishwa na vifo vya askari hao, lakini serikali ya umoja wa kitaifa nchini libya (GNA) imeishutumu Paris kwa "ukiukaji" wa ardhi yake, Jumatano, Julai 20.

Mabaki ya helikopta iliyokuwa ikiwasafirisha askari watatu wa Ufaransa, karibu na mji wa Benghazi, Julai 20, 2016.
Mabaki ya helikopta iliyokuwa ikiwasafirisha askari watatu wa Ufaransa, karibu na mji wa Benghazi, Julai 20, 2016. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya (GNA) imeiuhumu Ufaransa kwa "ukiukaji" wa ardhi yake katika ujumbe iliyoandika kwenye akaunti yake ya Facebook. GNA imekaribisha msaada unaotolewa na "nchi rafiki" lakini inaamini kwamba "hakuna kinachohalalisha kuigia katika ardhi yake" bila kupewa taarifa au bila kuratibu pamoja na serikali.

GNA imesema "kutofurahishwa natangazo la serikali ya Ufaransa kuhusu uwepo wa askari wa Ufaransa mashariki mwa Libya."

Kauli hii inafuata tangazo la Jumatano wiki hii lililotolewa na serikali ya Ufaransa kufuatia vifo vya askari watatu wa Ufaransa walipoteza maisha katika mazingira tatanishi wakiwa katika kazi ya serikali nchini Libya, tangazo ambalo limehibitisha kwa mara ya kwanza kuwepo kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini humo.

Maandamano dhidi ya "kuingiliwa kwa nchi za Magharibi" katika mji wa Benghazi

amami aya raia wa Libya waliandamana Jumatano hii katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wakipinga dhidi ya uwepo wa askari wa Ufaransa nchi mwao

Maandamano yalifanyika hasa katika eneo la Mashahidi mjini Benghazi, ambapo waandamanaji walidai mwisho wa "kuingiliwa na nchi za Magharibi katika yao" wito uliyotolewa ma Kiongozi wa kidini wa zamani wa Tripoli, Sadiq al-Ghariani.