DRC-MAI MAI-USALAMA

Mitwaba: Wanamgambo 3 wauawa katika mapigano na jeshi

Raia hawa wawili (picha) wameyakimbia makaazi yao kutokana na machafuko yanayoendelea Katanga, na kwa sasa wanaishi msituni.
Raia hawa wawili (picha) wameyakimbia makaazi yao kutokana na machafuko yanayoendelea Katanga, na kwa sasa wanaishi msituni. UNHCR/B.Sokol

Wanamgambo watatu wa kundi la waasi la Mai Mai waliuawa na wengine wawili walikamatwa Jumatano Julai 20 katika mapigano na askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) katika kijiji cha Busafa wilayani Mitwaba, mkoani (Katanga Kaskazini), makao makuu jeshi katika mkoa huo yamesema.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya kijeshi vinaarifu kuwa kuwa askari wanaimarisha ulinzi katika eneo hilo ambapo raia waliokimbilia wameanza kurejea.

Kwa mujibu wa vyanzo vya polisi wilayani Mitwaba, wapiganaji wa kundi la waasi la Mai Mai lilifanya mashambulizi katika mji wa Kalera Jumapili Julai 17 na kwa minajili ya kuwtorosha jela wenzao waliokamatwa wakati wamashambulizi ya hivi karibuni. Wauaji hao walikuta jela liko tupu. Wafungwa walikuwa walihamishiwa wilayani Mitwaba.

wakiwa ni wenye hasira, wapiganaji wa kundi la waasi Mai walichoma moto kituo cha polisi, na kumuua askari polisi mmoja kwa kumpiga risasi na mwili wake kuukata vipande vipande.

Wakati huo huo wanajeshi waliendesha operesheni ya kuwasaka. Pande hizi mbili zilipambana katika kijiji cha Busafa, na kufaanikisha kuwaua wanamgambo watatu wa kundi la waasi la Mai Mai.