DRC-UN

Kamishna mkuu wa UN wa Haki za Binadamu akamilisha ziara yake DRC

Zeid Ra'ad Zeid Al-Hussein, Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Oktoba 16 2014.
Zeid Ra'ad Zeid Al-Hussein, Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Oktoba 16 2014. REUTERS/Denis Balibouse

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu ameondoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katika ziara yake ya kikazi tangu mwanzo wa muhula wake, Zeid Ra'ad Zeid Al-Hussein alitembelea maeneo ya Kivu, miji ya Goma na Bukavu, na kumalizi ziara yake mjini Kinshasa, mji mkuu wa Congo.

Matangazo ya kibiashara

Alikutana na Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, maafisa wa usalama na vyama vya kiraia. Lakini hakukutana na Rais Joseph Kabila.

Katika mkutano wake na vyombo vya habari, alitoa wito wakuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa, ufunguzi wa mikutano ya hadhara kwa vyama vya kisiasa, akibaini kwamba bila hatua hiyo hakutakuwa na mazungumzo ya kuaminika. Hata hivyo amekaribisha maendeleo katika nyanja mbalimbali, ambayo ni juhudi ya serikali ya Kinshasa.

Ofisi ya Pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inaadhimisha miaka ishirini ya kuwepo ncini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema Al-Hussein.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Zeid Al-Hussein alielezea mambo nyeti yaliyoatekelezwa na serikali ya Kinshasa.Ahadi binafsi yarais Joseph Kabila katika kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia, hasa uliyotekelezwa na baadhi ya viongozi serikalini: maafisa 35 walihukumiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Bw Al-Hussein pia alisisitiza juhudi zenye thamani za serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasa ya Congo katika uchunguzi na mashtaka dhidi ya askari wa Congo waliokuwa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa wanaoshutumiwa uhalifu mbalimbali, hasa ubakaji nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Amesema ni jambo la kusifiwa, kwani hata baadhi ya nchi zinasita kufanya hivyo.

Ndiyo kwa mazungumzo ya kisiasa, lakini lazima kuwepo na maendeleo

Zeid Al-Hussein amesema alitembelea kwa mara ya kwanza nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2004 na amekaribisha maendeleo aliyoyakuta. Hata hivyo, amesema, maendeleo haya yako hatarini. Kutokuwepo kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya kisiasa, kutumiwa kwa vyombo vya sheria, ni miongoni mwa mambo ambayo yatasababisha maendeleo hayo kutoweka, amesema Al-Hussein.

Zeid Al-Hussein amesema kuunga mkono jitihada za mazungumzo za Rais Kabila, lakini mazungumzo haya "haiwezekani katika mazingira kama haya ambapo hali ya siasa ni tete, huku vyombo vya habari binafsi vikiminywa".