TANZANIA

Chama tawala nchini Tanzania kuamua mwenyekiti mpya

Halmashauri Kuu ya Chama tawala nchini Tanzania CCM imelijadili na kulipitisha jina la Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenda katika mkutano mkuu maalum kumchagua kuwa mwenyekiti mpya wa Chama hicho.

Mwenyekiti wa sasa wa CCM na Rais Mstaafu awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwenyekiti wa sasa wa CCM na Rais Mstaafu awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete. rfi
Matangazo ya kibiashara

CCM kitaendesha mkutano wake mkuu maalum leo jumamosi mjini Dodoma ambapo mkutano huo utamchagua mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.

Iwapo Mkutano huo mkuu maalum utachagua Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM atakabiliwa na changamoto za kukinganisha na kukisuka upya chama hicho.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa Mwenyekiti ajaye wa CCM atawajibika kuleta mabadiliko ndani ya Chama na kukiresha mikononi mwa wanachama.