DRC-ETIENNE TSHISEKEDI

DRC: Tshisekedi arejea Kinshasa Jumatano hii

Wafuasi wa UDPS wakijiandalia kurejea nchini kwa Etienne Tshisekedi Julai 27, 2016.
Wafuasi wa UDPS wakijiandalia kurejea nchini kwa Etienne Tshisekedi Julai 27, 2016. RFI/Habibou Bangré

Baada ya miaka miwili ya kutokuwepo nchini mwake, Etienne Tshisekedi anatazamiwa kurejea Jumatano hii Julai 27 mjini Kinshasa. Mpinzani huyu wa kihistoria anatazamiwa kuwasili kwa ndege ya kukodi mchana katika uwanja wa ndege wa Ndjili.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imetolewa na chama chake cha UDPS, ambacho kimekua kikihamasisha wafuasi wake kwenda kumpokea katika uwanja wa ndege. Mjini Kinshasa, maandalizi kwa ajili ya kurudi kwa Etienne Tshisekedi yanaendelea vizuri.

Katika maeneo mbalimbali ya mji wa Kinshasa, hasa kutoka uwanja wa ndege hadi nyumbani kwake katika kata ya Limete, Tshesekedi ni maarufu. Jumanne mchana tayari, watu walionekana wakiwa na uhakika kwamba kurejea kwake nchini kutapelekea hali ya nchi kuboreka zaidi: ahadi ya kupishana madarakani, kuheshimu haki za raia. wale wanojulikana kama "wapiganaji", lakini pia wanawake, wakiwa na furaha ya kumuona.

Katika maeneo mengine ya mji mkuu, wengi wanaona kuwa kurudi kwake nchini ni muhimu kwa ajili ya kupambana kisiasa kwa upande wa upinzani hasa kwa upande wa mazungumzo. Katika safu ya vyama vinavyoiunga mkono serikali wanaona kwamba kurudi kwa mpinzani huyo si tukio lolote la ajabu, isipokuwa tu kama atajiunga na mazungumzo yaliyoitishwa na Joseph Kabila, kama alivyoahidi mwenyewe awali. Kwa kweli, itakuwa ni mtihani halisi kwa umaarufu wake baada ya miaka miwili ya kutokuwepo nchini. Kurejea kwake nchini katika siku za nyuma kulisababisha machafuko makubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo.

Hakuna kushiriki kwa sasa katika mazungumzo ya kitaifa

Kwa sasa, hakuna suala la kushiriki katika kamati ya maandalizi ambapo shughuli zimepangwa kuanza Jumamosi Julai 30. Chama cha UDPS kama vyama vingine vya upinzani vilimpinga msuluhishi Edem Kodjo,vikimtuhumu kuwa na upendeleo.