CAMEROON-RFI

Cameroon: Ahmed Abba, mwaka mmoja sasa akiwa jela

Ahmed Abba, mwandishi wa Idhaa ya Kihausa ya RFI katika mji wa Maroua, ametimiza mwaka mmoja sasa akiwa jela nchini Cameroon. Alikamatwa katika mji huo wa kaskazini mwa nchi Julai 30, 2015. Anatuhumiwa "kula njama katika vitendo vya kigaidi" na "kutotoa taarifa", katika taarifa zake kuhusu mashambulizi ya kundi la Boko Haram. Bado anasubiri hukumu yake.

Mwandishi wa Idhaa ya Kihausa ya RFI nchini Cameroon, Ahmed Abba.
Mwandishi wa Idhaa ya Kihausa ya RFI nchini Cameroon, Ahmed Abba. via facebook profile
Matangazo ya kibiashara

Julai 30, kwenye muda wa saa nane mchana, gari moja ya polisi iliegesha mbele ya ofisi ya manispaa ya jiji la Maroua. Kama waandishi wengine, Ahmed Abba, mwenye umri wa miaka 38, alikuja kuhudhuria mkutano wa usalama uliyoandaliwa na gavana wa mkoa, siku 8 baada ya mashambulizi mawili yaliyoukumba mji huo.

Muda mchache baadaye askari polisi walimuomba mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kihausa ya RFI katika mji wa Maroua kuwafuata. Kukamatwa kwake kulifanyika "bila upinzani wowote tena kwa upole," amesema shahidi wa tukio hilo. Ahmed Abba aliwekwa chini ya ulinzi kwa muda wa siku 15, kisha alihamishiwa kwenye makao makuu ya Idara ya upelelezi mjini Yaounde ambapo anazuiliwa hadi sasa. Hakuna mtu anayeweza kumuona, wala familia yake, wala mwanasheria wake, wala daktari, wakati ambapo alipowekwa jela alipigwa. Inabidi kusubiri miezi mitatu ili kupata taarifa zake. "Ahmed Abba yuko salama," Waziri wa Mawasiliano, Issa Bakary Tchiroma aliiambia RFI tarehe 30 Oktoba.

Tarehe 13 Novemba 2015, Ahmed Abba alihojiwa na wapelelezi kutoka Polisi. Wakati huo ndipo alipojua kwamba anashitakiwa kwa "kula njama katika vitendo vya kigaidi" na "kutotoa taarifa". anatuhumiwa kuwa aliwasiliana na wajumbe wa kundi la Boko Haram na kwamba hakuitaarifu serikali kwa yale aliyokusanya kama habari. Alihamishiwa kwenda gereza la mjini Yaounde ambapo sasa anazuiliwa mwezi. Bila uchunguzi wowote, Ofisi ya mashitaka iliiomba mahakama ya kijeshi kushughulikia kesi hiyo.

Kesi hiyo ilianza Februari 29, 2016. Kesi hii ilisikilizwa kwa muda wa miezi saba, ambapo mwanasheria wa Ahmed Abba aliomba mahakama kumuachilia huru kwa dhamna, lakini maombi hayo yalikataliwa.

Hakuna ushahidi, hakuna mashahidi

Mpaka sasa, Ahmed Abba amesikilizwa mara 4. Mahakama haijaweka wazi ushahidi wake, wala kusema kuwa ina mashahidi. Mwanasheria wake amesema faili ya kesi hiyo iko tupu. Kesi ya Ahmed Abba itasikilizwa tena Jumatano, Agosti 3, 2016.