LIBYAIS-USALAMA

Mashambulizi ya kwanza ya Marekani dhidi ya IS Sirte

Mapigano yarindima katika mji wa Sirte.
Mapigano yarindima katika mji wa Sirte. REUTERS/Goran Tomasevic

Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya (GNA), Fayez al-Sarraj, ametangaza Jumatatu hii Agosti 1 kwamba Marekani imeendesha mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za kundi la Islamic State katika makao yao makuu mjini Sirte, kwa ombi la afisi yake.

Matangazo ya kibiashara

"Mashambulizi ya kwanza ya Marekani dhidi ya ngome sahihi za kundi la Islamic State uamefanyika leo" kwa ombi la GNA, "na kusababisha hasara kubwa (kwa upande wa wanajihadi) mjini Sirte," kilomita 450 mashariki mwa mji wa Tripoli, amesema Bw Sarraj wakati wa hotuba yake iliyorushwa kwenye runginga ya taifa. Pentagon imethibitisha taarifa hiyo.

Kundi la Islamic State limekua likiendesha mauaji na mashambulizi ya hapa na pale katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Libya.

Mwezi Juni askari wasiopungua 34 wa vikosi vya Serikali waliuawa katika mapigano makali na wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Islamic State (IS) wanaozingira kwa miezi kadhaa eneo la katikati la ngome yao ya Sirte.

Siku ya Jumanne ilikua siku mbaya kwa majeshi ya Serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) tangu Mei 12 yalipoanza mashambulizi yao kwa lengo la kuudhibiti mji wa Sirte (kaskazini) unaodhibitiwa na wanajihadi.

Hayo yakijiri watu 29 waliuawa na na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko wa ghala la silaha katika mji wa mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli kufuatia makabiliano kati ya raia wanaobebelea silaha na wanamgambo.