AFRIKA KUSINI-SIASA

Raia wa Afrika Kusini wajiandaa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa

Raia wa Afrika Kusini watapiga kura siku ya Jumatano kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa.

Matangazo ya kibiashara

Ni uchaguzi unaofanyika kipindi hiki rais Jacob Zuma anayeongoza chama cha ANC, akiendelea kushtumiwa kuhusika na wizi wa fedha za umma.

Uchaguzi huo utawahusisha wapiga kura Milioni 26.3 watakao wachagua Mameya na viongozi wa Manispaa katika miji 278 nchini humo.

Chama cha ANC kimekuwa kikishinda idadi kubwa ya viti katika uchaguzi kama huu tangu kuanza kutawala mwaka 1994.

Rais Zuma amewasihi wapiga kura nchini humo kuwachagua wagombea wa ANC ili waendelee kuongoza katika miji hiyo.

Naye kiongozi wa chama cha upinzani cha EFF Julius Malema ambaye chama chake kitashiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi huu, ametoa wito kwa wananchi wa taifa hilo kuipa adhabu serikali kuwa kuipigia kura upinzani.