NIGERIA-USALAMA

Nigeria: hatari ya silaha ndogo ndogo

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mbele ya askari wake wakati wa sherehe ya Siku kuu ya "Army Day" Dansadau, Julai 13, 2016.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mbele ya askari wake wakati wa sherehe ya Siku kuu ya "Army Day" Dansadau, Julai 13, 2016. STRINGER / AFP

Nigeria inachangia 70% ya silaha ndogo ndogo haramu zinazozunguka mikononi mwa raia katika Afrika Magharibi, Umoja wa Mataifa umesema.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya silaha ndogo ndogo milioni 350 haramu ziko mikononi mwa raia nchi Nigeria, kwa mujibu wa Kituo cha Kikanda kwa ajili ya Amani na upokonyaji wa Silaha barani Afrika, shirika la Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, baadhi ya silaha hizi zinatokea nchini Mali na Libya, ambazo kwa sasa zinakabiliwa na machafuko.

Uwepo wa silaha nyingi haramu nchini Nigeria ni tishio dhidi ya usalama wa nchi, Kituo cha Kikaanda kwa ajili ya Amani na upokonyaji Silaha barani Afrika kimesema.

Kituo hiki kimebainisha kuwa mzunguko wa silaha ndogo ndogo haramu ni hatari zaidi wakati ambapo Nigeria inakabiliwa na migogoro tatu: mapigano yanayoendeshwa kaskazini mashariki na kundi la Boko Haram, mapigano katika jimbo la Niger Delta na mapigano kati ya watu wanaohamahama na wakulima.