Ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa nchini Tanzania na Kenya na manufaa yake

Sauti 20:56
Marais Joseph Kabila wa DRC na Yoweri Museveni, wa Uganda wakiwa mjini Kampala Agosti 04 2016.
Marais Joseph Kabila wa DRC na Yoweri Museveni, wa Uganda wakiwa mjini Kampala Agosti 04 2016. Ikulu ya rais Uganda

Makala haya yameangazia ziara ya Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault nchini Kenya na Tanzania, ziara inayolenga kuimarisha uhusiano kidiplomasia kati ya Ufaransa na nchi hizi mbili za Afrika Mashariki.Juma hili mataifa ya DRC na Uganda yamekubaliana kuhusu kuimarisha usalama wa eneo la mashariki mwa DRCongo ambako waasi wa Uganda wa ADF wamekuwa wakishutumiwa kuzorotesha usalama wilayani Beni, lakini pia tumeangazia Burundi kutupilia mbali mpango wa kupelekwa kikosi cha walinda wa UN wakati katika uga wa kimataifa tumegusia hali ya siasa za Marekani, inavyoendelea kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo.