SUDANI KUSINI-UNSC

Hakuna makubaliano ya UN kuhusu azimio juu ya Sudan Kusini

Askari wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wakipiga doria kwenye kambi yao, Julai 20, 2016.
Askari wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wakipiga doria kwenye kambi yao, Julai 20, 2016. REUTERS/Stringer

Mjini New York, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura Ijumaa hii Agosti 12 azimio juu ya Sudan Kusini kwa kuimarisha kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

NakaIa iliandikwa na Marekani, ambayo hasa imekua ikijihusisha na hali inayojiri nchini Sudan Kusini, inabaini kuimarishwa kwa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini (UNMISS), ikiwa ni pamoja na kutuma askari 4,000 wa ziada kama kikosi cha kuingilia kati. Kwani licha ya kusainiwa kwa mkataba wa amani ikiwa ni mwaka mmoja sasa, mapigano yaliyoibuka mwishoni mwa mwaka 2013 bado yanaendelea, ikiwa ni pamoja na machafuko mapya yaliyozuka mapema mwezi Julai katika mji mkuu, Juba.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulinatazamiwa kukutana Alhamisihii kwa kuandaa kupigia kura azimio hilo, na hakuna makubaliano yaliyofikiwa. Hata kama kila mtu anakubaliana umuhimu wa hali na haja ya kulinda raia, nchi 9 tu au 10, kwa jumla ya 15, zinapaswa kukubaliana juu ya nakala hii, ambapo baadhi ya maelezo ya kiufundi bado yanajadiliwa.

Kama inavyotaka IGAD, jumuiya ya amani na usama katika ukanda wa Afrika Masharikini, kikosi cha Umoja wa Mataifa chenye askari 12 000, kiinaweza kuimarishwa kwa kuwasili kwa askari 4 000 wa ziada, ikiwa ni sehemu ya muundo maalum kuwa wajibu na uwezo wa kupatanisha kati ya pande mbili zinazo hasimiana.

Pendekezo hilo la kuimarishwa kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini linaendelea kupindwa na serikali ya Juba. Baraza la Usalama pia linajadili kuhusu vikwazo vya silaha, lakini Marekani hasa haipendelei kuweka mbele vikwazo vya haraka.