ZAMBIA

Edgar Lungu aongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa raisi Zambia

Upinzani mkali ni kati ya Edgar Lungu na Hakainde Hichilema katika matokeo ya uchaguzi wa uraisi nchini Zambia
Upinzani mkali ni kati ya Edgar Lungu na Hakainde Hichilema katika matokeo ya uchaguzi wa uraisi nchini Zambia Emmanuel Makundi - RFI

Matokeo ya uchaguzi yanaendelea kutolewa nchini Zambia ambapo Rais Edgar Lungu anaongoza akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Hakainde Hichilema.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo kamili yanatarajiwa leo jumapili ambapo hadi sasa majimbo zaidi ya ishirini kati ya 156 yametangaza matokeo.

Hapo jana waangalizi wa uchaguzi walitoa wito wa utulivu kudumishwa baada ya madai ya ucheleweshwaji wa matokeo.

Tume ya taifa ya uchaguzi ilikanusha tuhuma kutoka kwa mgombea wa upinzani Hichilema, kwamba tume hiyo inashirikiana na chama tawala kuchelewesha matokeo.