AFRIKA KUSINI-MARIKANA

Marikana: hali ya maisha ya wachimbaji wa migodi bado ni ngumu

Wachimbaji wa madini ya Platinum katika mji wa Marikana mwezi Juni 2014.
Wachimbaji wa madini ya Platinum katika mji wa Marikana mwezi Juni 2014. REUTERS/Skyler Reid

Jumanne, Agosti 16, itakuwa maadhimisho ya miaka minne ya mauaji ya Marikana nchini Afrika Kusini. Wachimbaji wa migodi thelathini na wanne waliuawa kikatili na polisi wakati wa mgomo wa muda mrefu.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tume ya uchunguzi Farlam, kukosa makazi ya heshima kwa wachimbaji wa migodi wa kampuni ya Lonmin ni miongoni mwa sababu kuu za mgomo uliokua ukiendelea kwa miezi kadhaa nchini Afrika Kusini katika sekta ya madini, hasa katika kampuni ya Lonmin. Miaka minne baadaye,hakuna imebadilika yoyote yaliyoshuhudiwa: Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International limeweka wazi hali hiyo katika ripoti iliyotolewa Jumatatu hii.

Marikana, moja ya maeneo muhimu ya madini nchini Afrika Kusini, pia ni mmoja ya wauzaji wakuu wa Platinum duniani. Mapema mwezi Agosti 2012, mgodi wa Marikana ulikumbwa na migomo na vurugu zilizosababisha vifo vya watu wengi. Shughuli ya uchimbaji madini ilianzishwa tena mwezi Septemba, baada ya wiki tano za mgomo na kusainiwa kwa mkataba ikiwa ni pamoja na kuongezwa kwa mshahara.

Mgomo ulikuwa na lengo la kupata maboresho kutoka uongozi wa kampuni ya Lonmin katika mazingira ya kazi na maisha ya wachimbaji wa madini. Lakini miaka minne baadaye, "utaona tu kwamba wachimbaji wa madini wa Marikana wanaishi katika nyumba zilizojengwa kwa bati au mbao; hawana kitu chochote, amesema Deprose Muchena, Mkurugenzi wa Amnesty International nchini Afrika Kusini. Familia hizi zinaishi katika maisha duni ya kusongamana: hakuna maji ya bomba. Na kama wana umeme, wanaupata kwa haramu, na katika majira ya baridi, ni tatizo kwa familia kwa sababu vibanda vyao haviwalindi kwa baridi. Kampuni ya Lonmin inasema kuwa takriban wafanyakazi 13 500 miongoni mwa wafanyakazi wake hawana nyumbani halisi, ni hali ambayo inatisha. "

Kwa mujibu wa hati iliyotolewa na Amnesty, mgodi wa huo una wafanyakazi wa kudumu 20,000 katika mji wa Marikana na zaidi ya nusu ni wafanyakazi wa kigeni. Kampuni ya Lonmin inawahifadhi kimalazi wafanyakazi 3,000 na wengine wanaosalia wanajitegemea.