DRC-BENI-USALAMA

DRC: Serikali yatangaza amri ya kutotoka nje usiku Beni na Butembo

Maduka yafungwa Beni, Agosti 18, 2016.
Maduka yafungwa Beni, Agosti 18, 2016. RFI / Sonia Rolley

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza Alhamisi hii, Agosti 18, amri ya kutotoka nje usiku katika miji ya Beni na Butembo, mashariki mwa nchi hiyo, baada ya maandamanoya Jumatano wiki hii dhidi ya serikali.

Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa miji hiyo wametakiwa kutotoka nje kuanzia saa moja usiku gadi saa kumi na mbili asubuhi. Tangazo hili limetolewa na Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani, Evariste Boshab. Hatua ambayo haikuwaridhisha wafanyabiashara. Wafanyabiasha katika mji wa Beni waliamua Alhamisi hii kufunga maduka yao katika barabara kuu ya Nyamwisi. Wafanyabiashara wanaomba kuachiwa huru kwa waandamanaji wanaozuiliwa.

Katikati mwa mji wa Beni, maduka yalifungwa Alhamisi hii Agosti 18 kwenye barabara kuu ya Nyamwisi ambapo ni moja ya meneo kulikofanyika maandamano ya Jumatano. Wafanyabiashara wameeleza kwamba bado wanaomboleza wahanga wa tukio hilo. kuu wa mji wa Beni alisema kuwa mtu mmoja ndio aliyeuawa kwa risasi na askari polisi aliyeuawa kwa kupigwa mawe. Mtu mwengine aliuawa katika maandamano hayo, idadi hii ni kubwa mwa raia, amesema mmoja wa wafanyabiashara.

Wafanyabiasaha wanadai pia kuachiwa huru kwa waandamanaji wote na kurejeshwa kwa vifaa vya viliyopokonywa na vikosi vya usalama. Hatutofungua maduka kama madai yetu hayatopatiwa ufunbuzi, amesema mfanyabiashara mmoja. Mfanyabiasha mwingine amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna uwezekano raia kuingia tena mitaani.

Kabla ya kuondoka, Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani alisema kuwa watu waliokamatwa watahojiwa na kisha waachiliwe. Evariste Boshab alisema alipewa taarifa ya watu saba waliokamatwa. Lakini asasi za kiraia, zinasema kuwa zina idadi ya waandamanaji 148 wanaozuiliwa, ikiwa ni pamoja na watoto 15 na wanawake 36.