MALI-USALAMA

Mali: Mohamed Youssouf Bathily aachiwa kwa dhamana

Vizuizi vilivyowekwa baada ya makabiliano kati ya waandamanaji na vijosi vya usalamaAgosti 17, 2016 mjini Bamako.
Vizuizi vilivyowekwa baada ya makabiliano kati ya waandamanaji na vijosi vya usalamaAgosti 17, 2016 mjini Bamako. HABIBOU KOUYATE / AFP

Vymvo vya sheria nchini Mali vimemuachia huru kwa dhamana Mohamed Youssouf Bahtily, anayejulikana kwa jina maarufu la "Ras Bath", ambaye alikua akishtumiwa na serikali makosa mbalimbali , ikiwa ni pamoja na mpango wa kuhatarisha usalama wa taifa.

Matangazo ya kibiashara

Mohamed Youssouf Bathily, ambaye ni mtoto wa Waziri wa sasa wa Masuala ya Ardhi, Mohamed Ali Bathily, anajulika kwa ajili ya upinzani wake mkali dhidi ya serikali, viongozi waandamizi wa utawala na jeshi la Mali.

Mohamed Youssouf Bathily alishtakiwa kwa kosa la udhalilishaji wa Mila na kauli ambayo ingeliweza kusambaratisha vikosi vya jeshi vya Mali.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Mali, Mohamed Youssouf Bathily ameachiwa kwa dhamana baada ya upatanishi wa baadhi ya viongozi wa dini wenye ushawishi mkubwa nchini Mali.

Wakati huo huo serikali imetoa idadi ya watu waliopoteza maisha pamoja na uharibifu wa mali wakati wa maandamano ya Jumatano Agosti 17 mjini Bamako. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Waziri wa Usalama wa Mali, Salif Traoré, vurugu zilizotokea hivi katibuni nchini Mali, zilisababisha kifo cha mtu mmoja, na wengine 18 kujeruhiwa ikiwa ni pamoja na askari polisi 4, huku mali nyingi zikiharibiwa.