Serikali ya DRC yajiapiza kutokomeza ADF wilayani Beni

Sauti 22:26
Waziri mkuu wa DRC Matata Ponyo (kulia) akiteta kitu na manusura wa mauaji ya Beni usiku wa Agosti 13 kuamkia Agosti14 2016.
Waziri mkuu wa DRC Matata Ponyo (kulia) akiteta kitu na manusura wa mauaji ya Beni usiku wa Agosti 13 kuamkia Agosti14 2016. RFI/Sonia Rolley

Makala ya mtazamo wako kwa yaliyojiri wiki hii imeangazia mauaji ya watu zaidi ya hamsini katika kata ya rwangoma mjini Beni DRC na mikakati ya serikali katika kuwatokomeza waasi wa Uganda wa ADF wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo, na tume ya umoja wa mataifa, Monusco imemsafirisha kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar hadi DRCongo kabla ya kuelekea Ethiopia, pia tumeangazia siasa za Burundi, Kenya, na Tanzania.Kimataifa tumetupia jicho ziara ya rais wa Urusi Vladmir Putin huko Crimea jimbo lililojitenga na Ukraine.Kusikiliza zaidi, ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka Ben Saleim.