MALAWI-SHERIA

Malawi: Waziri wa zamani ahukumiwa

Moja ya vijiji nchini Malawi.
Moja ya vijiji nchini Malawi. Pixabay/CC/Public domain

Mahakama Kuu mjini Lilongwe Jumanne hii, imewmuhukumu Waziri wa zamani wa sheria, Raphael Kasambara, kifungo cha miaka 13 jela na kuamurishwa kufanya kazi ngumu kwa kosa la kula njama kwa mauaji.

Matangazo ya kibiashara

Bw Kasambara amepatikana na hatia ya kula njama katika mauaji mwezi Septemba 2013 ya mkurugenzi wa zamani wa Bajeti katika Wizara ya Fedha, Paul Mphwiyo.

Mauaji ya Bw Mphwiyo yalipelekea ugunduzi wa kashfa ya uporaji wa rasilimali za umma wakati wa utawala wa Rais Joyce Banda, kashfa ambayo ilibatizwa jina la "cashgate".

Karibu milioni 250 zililipwa kwa udanganyifu kwa wafanyabiashara kwa ajili ya huduma ambazo hazikuwahi kufanyika.

Siku chache kabla ya kashafa hiyo, afisa mkuu wa serikali alikutwa na dhahabu nyingi zinazomilikiwa na mamlaka ya Hazina ya Serikali, sawa na zaidi ya dola za Marekani milioni 300, ndani gari lake.

Fedha hizo pia zilihifadhiwa ya magari nyumbani kwa baadhi ya maafisa wa serikali.

Mara tu baada ya hukumu dhidi yake mwezi uliopita, Kasambara aliarifu kuwa kamwe hatakata rufaa wa uamuzi wa Mahakama.