Pata taarifa kuu
VATICAN

Kanisa katoliki lamtangaza Mother Teresa kuwa mtakatifu

Mama Teresa akiwa nje ya makao makuu ya kituo cha misaada cha kanisa katoliki mjini Kolkata nchini India, picha ilipigwa siku chache kabla ya kufariki kwake September 5, 1997.
Mama Teresa akiwa nje ya makao makuu ya kituo cha misaada cha kanisa katoliki mjini Kolkata nchini India, picha ilipigwa siku chache kabla ya kufariki kwake September 5, 1997. Stringer/REUTERS/File photo
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi
2 Dakika

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis, Jumapili ya Agosti 4, 2016, amemtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu, akisifu kazi alizozifanya mjini Kolkata India, kwa ni zaidi ya ubinadamu na upendo wa Mungu aliokuwa nao kwa kuwasaidia watu masikini.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe za kumtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu zilifanyika kwenye ibada maalumu ya utakaso kwenye uwanja wa St Peters, ikiongozwa na Papa Francis mbele ya waumini zaidi ya laki moja waliohudhuria.

“Kwa heshima kubwa...tunamtangaza na kumueleza mbarikiwa Teresa wa Calcutta (Kolkata) kuwa mtakatifu na kumuingiza kwenye orodha ya watakatifu, na kwamba ameidhinishwa na kanisa zima la katoliki”. Alisema Papa Francis.

Papa Francis amesema kuwa licha ya kumtangaza kama mtakatifu, bado ataendelea kubaki kuwa Mama Teresa kwa kanisa katoliki.

Papa Francis akiongoza moja ya ibada alizozifanya hivi karibuni, amemtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu
Papa Francis akiongoza moja ya ibada alizozifanya hivi karibuni, amemtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu REUTERS/Stefano Rellandini

Akipasa sauti yake na maono yake kuwa “kanisa masikini kwa watu masikini” papa Francis ameelezea kasi za Teresa kama kielelezo cha usafi wa matendo ya Mungu kwa watu masikini.

Akinukuu maneno aliyowahi kuyasema Mama Teresa wakati wa uhai wake, papa Francis amenukuu akisema “Mama Teresa alipenda kusema, hata kama sifahamu lugha yao lakini naweza kutabasamu’.

“Hebu tuchukue tabasamu lake na kuliweka mioyoni mwetu na kuwapa wale ambao tutakutana nao njiani hasa wale ambao wana taabika.”

Papa Francis alitumia ibada hiyo pia kusifu msimamo wa Mama Teresa wa kupinga kitendo cha utoaji mimba “ambacho kilibainishwa na Mama Teresa kama mauaji” na kushinda tuzo la Nobel mwaka 1979.

Ibada hii maalumuj imefanyika siku moja kabla ya maadhimishi ya 19 ya kifo cha Mama Teresa mjini Kolkata, mji wa India ambako Teresa aliishi huko kwa karibu miongo minne akifanya kazi kwenye maeneo ya watu masikini zaidi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.