SOMALIA

Nchi ya Somalia yashinikizwa kulinda uhuru wa vyombo vya habari

Umoja wa Mataifa umeitaka Serikali yha Somalia kufanya zaidi kulinda uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza, kwenye taifa ambalo mpaka sasa waandishi wa habari zaidi ya 30 wameuawa katika kipindi cha miaka 4.

Moja ya kituo cha Redio nchini Somalia, ambako wanahabri wako hatarini zaidi kuuawa.
Moja ya kituo cha Redio nchini Somalia, ambako wanahabri wako hatarini zaidi kuuawa. UN Photo/Tobin Jones
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo ripoti ya umoja wa Mataifa licha ya kueleza hofu iliyopo, imeonesha kupigwa hatua japo kidogo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.

Ripoti hii ambayol imeandikwa kwa pamoja na tume ya umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM pamoja na tume ya umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, imeeleza kufurahishwa na kupitishwa kwa muswada wa sheria iliyosema angalau unatia matumaini na kutoa hakikisho la uhuru kwa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa.

Ripoti hiyo pia, imeonesha kuguswa na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye muswada huo wa sheria, ambayo inasema hayaleti mantiki nzuri na kuruhusu mtu kutafsiri kwa namna nyingine na baadhi ya sheria kutoruhusu uhuru wa vyombo vya habari.

“Licha ya utamaduni mzuri wa vyombo vya habari nchini Somalia, taifa ambalo lina vyombo vya habari zaidi ya 90 ikiwemo Blogs na na mitandao, matukio kadhaa ua ukiukwaji wa haki za binadamu kwa waandishi wa habari, yameanishwa kwenye ripoti hiyo.

Matukio hayo ni pamoja na mauaji, mashambulizi, kukamatwa na kuwekwa kizuizini, vitisho, unyanyasaji, kufungwa kwa ofisi za baadhi ya vyombo vya habari, kushikiliwa kwa vifaa na mali pamoja na kuzuia baadhi ya tovuti.

Ripoti inasema kuwa kati ya mwezi Agosti mwaka 2012 na Juni 2016, jumla ya wanahabari 30 na wabunge 18 waliuawa nchini Somalia.

Wakati kitisho kikubwa kwa wanahabari nchini Somalia kikiwa ni kutoka kwa kundi la Al-Qaeda na wanamgambo wa Al-Shabab ambao wameapa kuiangusha Serikali, vyombo vya usalama pia vina hatia ya matukio kadhaa ya unyanyasaji na mauaji dhidi ya wanahabari na wanasiasa.