SUDANI KUSINI-UNSC

Sudan Kusini yakubali kutumwa kwa askari wa kulinda amani wa ziada

Askari wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wakipiga doria kwenye kambi yao, Julai 20, 2016.
Askari wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wakipiga doria kwenye kambi yao, Julai 20, 2016. REUTERS/Stringer

Serikali ya Sudan Kusini imekubali Jumapili hii kutumwa kwa askari wa kulinda amani 4,00 wa ziada nchini mwake, serikali imebaini katika tangazo lililoandikwa kwa pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini Juba.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni, Rais Salva Kiir alikataa katu katu kuwepo kwa askari wa kulinda amani 4,000 wa ziada nchini Sudan Kusini.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumamosi hii Agosti 3, lilitoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kuacha upinzani wake kuhusu kupelekwa kwa kikosi cha kikanda cha kuimarisha ulinzi katika ujumbe wa askari wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani katika nchi hiyo inayokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mabalozi kutoka nchi 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walikutana na Mawaziri waandamizi wa serikali mjini Juba na wote walizungumzia kuunga mkono pendekezo la kutumwa kwa wanajeshi 4,000 wa ziada kwa kikosi cha askari 13,000 wa UNMISS waliomo nchini humo.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power baada ya kuwasili mjini Juba, alisisitiza kwamba askari 4,000 wa ziada wa kulinda amani kutoka Afrika wanahitajika.

Muswada wa kikosi hiki cha ulinzi ulianzishwa na nchi za Afrika Mashariki, na majina ya Kenya, Rwanda na Ethiopia yameendelea kutajwa kwa wiki kadhaa kama nchi ambazo ziko tayari kuunda kikosi hiki.

Mapigano makali ya Julai 8 hadi 11 katika mji wa Juba kati ya wanajeshi wa rais Salva Kiir na wale wa kiongozi wa zamani wa waasi, Riek Machar yamesababisha hali ya usalam kuwa tete nchini Sudani kusini.

Mapigano haya ambayo yalisababisha vifo vya watu wengi na wengine wengi kujeruhiwa, yalipelekea Riek Machar kukimbilia uhamishoni. Bw Machar alikua aliiombajumuiya ya kimataifa kuimarisha tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), akibaini kukosa uwezo wa kulinda raia mwezi Julai.