UCHAGUZI-GABON

Wataamu wasema wizi wa kura barani Afrika waelekea kukoma

Waandamanaji raia wa Gabon wakiandamana jijini Paris, Ufaransa, September 3, 2016
Waandamanaji raia wa Gabon wakiandamana jijini Paris, Ufaransa, September 3, 2016 Thomas SAMSON / AFP

Wakati huu nchi ya Gabon ikikabiliwa na machafuko ya mara baada ya uchaguzi mkuu ulioshuhudia kurejea madarakani kwa Rais Ali Bongo Ondimba, wataalamu wanasema kuwa udanganyifu wa chaguzi barani Afrika unazidi kuwa mgumu, shukrani kwa mashirika ya kijamii ambayo yamekuwa yakifuatilia chaguzi mbalimbali na kukosoa pamoja na kuenea kwa teknolojia ya simu za mkononi.

Matangazo ya kibiashara

Ijumaa ya wiki iliyopita, kiongozi mkuu wa upinzani nchini Gabon, Jean Ping alijitangaza kuwa mshindi na Rais halali wa Gabon na kutaka kurudiwa upya kwa uhesabuji wa kura, kufuatia madai ya Rais Bongo kudai kuwa aliibuka mshindi kwa zaidi ya kura elfu 6 katika uchaguzi wa Agosti 27 mwaka huu.

Lakinik chaguzi za hivi karibuni nchini Nigeria, Ivory Coastm Benin na Burkina Faso zimefanyika bila ya kuwepo kwa udanganyifu mkubwa, ukitazamwa kwa kuwashirikisha raia waliohakiki zoezi zima la uchagizi wenyewe.

Mathias Hounkpe, meneja wa taasisi ya siasa na utawala wa Afrika Magharibi OSIWA, anasema kuwa kadri miaka inavyozidi kwenda, udanganyifu kwenye uchaguzi unazidi kuwa mgumu kufanywa na viongozi walioko madarakani.

Waandamani raia wa Gabon waandamana barani Ulaya.
Waandamani raia wa Gabon waandamana barani Ulaya. Thomas SAMSON / AFP

Uwepo wa waangalizi wa ndani na wale wa kimataifa, pamoja na uwepo wa tume huru zisizofungamana na upande wowote, vimechangia kwa sehemu kubwa kuruhusu kufanyika kwa chaguzi zilizokuwa huru na za haki na kuzuia wizi na udanganyifu wa kura au kubadilisha matokeo.

Aboubacry Mbodji, katibu muuu wa shirika la haki Afrika RADDHO katika nchi za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati, anasema kwa sehemu kubwa chaguzi kwenye nchi kama vile za Ghana, Senegal na visiwa vya Cape-Verde, inaonesha bara la Afrika linabadilika na kuelekea kufanya chaguzi za wazi na haki.

Mashirika ya kijamii, uwepo wa vyombo vya habari na urahisi wa wananchik kutumia teknolojia ya mawasiliano kusambaza taarifa, ni kichocheo tosha kilichofanya chaguzi nyingi sasa barani Afrika kufanyika kwa uhuru na uwazi.