Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UN-MACHAR

UN yahofia uwepo wa waasi wa Sudan Kusini waliokimbia DRC

Waasi wa Sudan Kusini wanaomuunga mkono Riek Machar, Machi 2016, mjini Juba.
Waasi wa Sudan Kusini wanaomuunga mkono Riek Machar, Machi 2016, mjini Juba. Getty Images
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Uwepo wa waasi wa Sudan Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kunaweza kutishia utulivu wa unaoshuhudiwa katika ukanda huo, Umoja wa Mataifa umesema.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) unasema kutiwa wasiwasi kuhusu uwepo nchini DRC wa wapiganaji wa Sudan Kusini wanaomuunga mkono kiongozi wa waasi Riek Machar.

Takriban waasi mia nane wa Sudan Kusini wanapatikana kwa sasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO imebaini na kuongeza kuwa waliweka chini silaha zao j walipowasili nchini DR Congo.

"Tunaamini kwamba serikali husika na mashirika ya kiukandal yatafanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha kuwa amani na usalama vinazingatiwa katika ukanda huu, " Msemaji wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini DR Congo (MONUSCO), Charles Bambara ameiambia BBC .

Umoja wa Mataifa nchini DRC "unawasadia" raia wa Sudan Kusini waliowasili katika ardhi ya DR Congo "tangu Agosti 17, kwa ombi la Serikali ya DRC," amebainisha Bambara.

Riek Machar na wapiganaji wake walikimbilia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya mapigano makali yaliyotokea mwezi Julai 2016 mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Machar aliondoka nchini DRC na kuelekea nchini Sudan, ambapo alipatishiwa matibabu, kwa mujibu wa viongozi wa Sudan.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.