Pata taarifa kuu
DRC-JOSEPH KABILA

Wanaharakati wa kisiasa 16 wazuiliwa kinshasa

Msemaji wa serikali ya Kinshasa Lambert Mende
Msemaji wa serikali ya Kinshasa Lambert Mende

Takribani wanaharakati 16 wa upinzani nchini DRCongo wanazuiliwa jijini Kinshasa baada kukutana na kujadili namna ya kumzuia raisi kabila kusalia madarakani kinyume cha katiba daaba ya muda wake kutamatika,umoja wa mataifa umefahamisha.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa kitengo cha haki za binadamu katika umoja wa mataifa nchini DRC Jose-Maria Aranaz amesema takribani wanaharakati wa upinzani 16 walikamatwa kati ya alhamisi na ijumaa asubuhi baada ya mkutano wa kujadili kuheshimiwa kwa katiba ya congo na kukabidhi madaraka.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limetuhumu mamlaka nchini DRC kufanya unyanyasaji dhidi ya watu wanaodai kuondoka kwa raisi kabila mara baada ya muda wake kutamatika madarakani December 20.

Msemaji wa serikali Lambert Mende ameshangazwa na madai hayo akisema kuwa mamlaka ilikuwa imeachia wanaharakati kadhaa wa kisiasa mnamo mwezi August.

Kabila, ambaye ameiongoza DR Congo tangu mwaka 2001,anazuiliwa na katiba ya taifa hilo kuwania tena lakini hakuna ishara za nia ya kukabidhi madaraka mwezi Decemba.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.