GABON

Mahakama ya katiba nchini Gabon kuamua hatma ya Ping na Rais Bongo

Mawakili wa Rais Ali Bongo wa Gabon pamoja na wale wa mpinzani wake, Jean Ping, wanakutana kwenye mahakama ya katiba, tayari kuanza kusikilizwa mara ya kwanza kwa shauri la upingaji wa matokeo yaliyompa ushindi rais Bongo.

Mahakama ya Katiba ya Gabon haitaki msaada wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa uchaguzi.
Mahakama ya Katiba ya Gabon haitaki msaada wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa uchaguzi. © (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Shauri hili linaanza kusikilizwa Alhamisi ya September 22, siku moja tu kabla ya muda wa mwisho wa siku 15 uliowekwa kikatiba kwa shauri hilo kuwa limetolewa uamuzi na mahakama ya kikatiba.

Rais Bongo alitangazwa mshindi baada ya uchaguzi wa Agosti 27, ambapo alishinda kwa idadi ndogo ya kura ambazo zilikuwa chini ya elfu 6, ushindi ambao ulizusha machafuko ya siku kadhaa upinga ushindi wake.

Upinzani ulipinga kura hiyo kwa madai ya udanganyifu September 8 mwaka huu, ambapo Ping mwanadiplomasia anayeheshimika kimataifa, alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo, ambapo alifungua kesi kutaka kuhesabiwa upya kwa kura.

Uamuzi wa mahakama ya katiba unatarajiwa kutolewa September 23 mwaka huu baada ya kusikiliza pande zote mbili.

Mawakili wa Ping wamethibitisha kupokea wito wa mahakama, ambao uliwataka kufika mahakamni siku ya Alhamisi kuanza kusikiliza shauri lao.

Waangalizi watawasilisha ripoti yao na kisha mawakili wa pande zote watazungumza kwa dakika 10, alisema wakili anayemwakilisha Rais Ali Bongo.

Hata hivyo haijafahamika ikiwa mahakama hiyo ya katiba itatoa uamuzi Alhamisi hii au itatoa uamuzi wa jumla ifikapo Ijumaa ya September 23.

Ping anataka kuhesabiwa upya kwa kura zote kwenye ngome ya rais Bongo kwewnye mji wa Haut-Ogooue, ambako alishinda kwa zaidi ya asilimia 95, eneo ambalo limeripotiwa kuwa watu waliojitokeza walikuwa ni zaidi ya asilimia 99.

Jumanne ya wiki hii, mawaikili kutoka pande zote mbili walikubaliana kuhesabiwa upya kwa kura kwenye mji wa Haut-Ogooue ingawa hawakukubaliana kuhusu njia watakayotumia.

Hata hivyo Ping anasema kuwa hana imani na mahakama hiyo kwakuwa mahakama nyingi ameziweka mfukoni mwaka, akitolea mfano rais wa mahakama hiyo ambaye amedai alikuwa kimada wa baba yake.