FARU-TEMBO-CITES

Mataifa yavutana kuhusu kukaza ama kulegeza masharti kuhusu biashara ya viumbe vilivyo hatarini

Chaque année, le nombre de rhinocéros tués augmente en Afrique du Sud.
Chaque année, le nombre de rhinocéros tués augmente en Afrique du Sud. AFP PHOTO / STEPHANE DE SAKUTIN

Kupungua kwa faru na tembo barani Afrika, ambao meno na pembe zao zinalengwa na majangili, inatarajiwa kugubika mjadala wa siku 12 jijini Johannesburg wakati wa kongamano la kimataifa kuhusu biashara na viumbe walioko hatarani kutoweka, CITES, mkutano unaong’oa nanga mwishoni mwa juma.

Matangazo ya kibiashara

Uwindaji na biashara haramu ya wanyama pori inakadiriwa kufikia thamani ya dola za Marekani bilioni 20 kwa mwaka, hii ni kwa mujibu wa shirika la umoja wa Mataifa la CITES, ambapo limeorodhesha biashara hii kuwa biashara haramu ya nne kwa ukubwa dunia baada ya ile ya uuzaji wa silaha, bidhaa na usafirishaji wa binadamu.

Wajumbe wanaoshiriki kwenye kongamano hili, watajadiliana na pengine kuamua ikiwa waongeze masharti zaidi dhidi ya biashara hii ama kuyalegeza kwa viumbe 500 ambao ni wanyama na mimea.

Katibu mkuu wa CITES, John Scanlon amesema kuwa, lengo kubwa la jumuiya ya kimataifa ni kutazama biashara ya pembe za ndovu barani Afrikana pia faru weupe wanaopatikana kwenye pembe ya nchi za kusini mwa Afrika pamoja na kukomesha biashara hiyo.

Sehemu ya shehena ya meno ya tembo iliyoteketezwa hivi karibuni nchini Kenya.
Sehemu ya shehena ya meno ya tembo iliyoteketezwa hivi karibuni nchini Kenya. REUTERS/Thomas Mukoya

Shirika hili la umoja wa Mataifa, lilitangaza kupiga marufuku biashara ya pembe za faru miaka 40 iliyopita, lakini licha ya makataa hayo, biashara hiyo haijakoma wala kupunguam huku ikikithiri kwenye nchi ya Afrika Kusini.

Zaidi ya faru weupe elfu 5 ikiwa ni sawa na robo tatu ya faru wote, wameuawa katika kipindi cha miaka 8 iliyopita, huku wengi wakiuawa nchini Afrika Kusini, nchi ambayo ni hifadhi ya karibu asilimi 80 ya faru weupe duniani.

Biashara ya pembe za faru inachochewa na mahitaji makubwa ya wafanyabiashara kutoka Vietnam na Uchina, maeneo ambayo watumiaji wake wana imani kuwa ni dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali.

Nchi ya Swaziland inataka kutumia kongamano hili kutaka kulegezwa kwa masharti ya biashara hii ya pembe za ndovu, ili kutoa nafasi kwa nchi hiyo kuuza mamilioni ya shehena za makontena ya pembe zilizokamatwa.

Wazo la Swaziland limeungwa mkono na baadhi ya nchi za Ulaya na Amerika, ambazo zinasema kuwa ili kukomesha soko haramu la pembe za faruj na meno ya tembo, basi dunia ilegeze masharti na kuruhusu kuuzwa kwa shehena ambazo zinashikiliwa hadi pale zitakapoisha.