MAREKANI-DRC

Marekani yaendelea kuwachukulia vikwazo maafisa wa jeshi la DRC

Jenerali Gabriel Amisi Kumba maarufu "Tango Fort" (katikati), hapa mwaka 2004.
Jenerali Gabriel Amisi Kumba maarufu "Tango Fort" (katikati), hapa mwaka 2004. AFP PHOTO/HELEN VESPERINI

Serikali ya Marekani imewachukulia vikwazo ma jenerali wawili kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo kufuatia mwenendo wao dhidi ya wananchi wa taifa hilo. Baada ya jenerali Kanyama kuwekewa vikwazo mwezi Juni mwaka huu, sasa ni zamu ya jenerali Gabriel Amisi Kumba maarufu Tango Fort pamoja na John Numbi Banza Tambo.

Matangazo ya kibiashara

Mali za viongozi hao wa jeshi zilizo hifadhiwa Marekani zimezuiliwa na hakuna raia yeyote wa Marekani anaeruhusiwa kufanya shughuli za ubadilishanaji wa fedha na viongozi hao.

Kwa mujibu wa John Smith mkurugenzi wa idara ya Marekani iliotangaza vikwazo hivyo amesema jenerali Amisi Kumba anatuhumiwa kutumia nguvu zaidi wakati wa kuzima maandamano ya kisiasa yaliyofanyika Januari mwaka jana jijini Kinshasa. Jenerali Numbi anatuhumiwa kutumia vitisho katika uchaguzi wa March dhidi ya wafuasi wa upinzani kwa faida ya vyama vinavyomuunga mkono Rais Kabila.

Wakati hayo yakiarifiwa, Waziri wa Sheria nchini DR Congo Alexis Tambwe Mwamba amesema maandamano yaliofanyika septemba 19 mwaka huu hayakuwa ya amani na kwamba matukio mengi yaliyotekelezwa na wafuasi wa upinzani hayawekwi wazi na vyombo vya habari vya kimataifa.

Utawala na upinzani wameendelea kunyoosheana kidole cha lawama, kila mmoja akimtuhumu mwingine kuhusika katika vurugu na mauaji yaliotokea katika maandamano ya Septemba 10 na 20 mwaka 2016.