MISRI-USALAMA

Afisa wa Muslim Brotherhood auawa na polisi

Kwa mujibu wa polisi ya Misri, Mohamed Kamal aliuawa wakati wa kukamatwa kwake.
Kwa mujibu wa polisi ya Misri, Mohamed Kamal aliuawa wakati wa kukamatwa kwake. REUTERS/Muhammad Hamed

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imetangaza kwamba polisi ya Misri ilimua kwa kumpiga risasi kiongozi wa tawi la "operesheni maalum" za kundi la Muslim Brotherhood. Mohamed Kamal na walinzi wake waliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa kukamatwa kwao, polisi imesema.

Matangazo ya kibiashara

Mohamed Kamal alikuwa mmoja wa watu muhimu wa kundi la Muslim Brotherhood kwani alikua mjumbe wa kamati kuu ya kundi hilo yenye majukumu ya kumteua kiongozi mkuu wa kundi la Muslim Brotherhood.

Kiongozi mkuu wa sasa wa kundi la Muslim Brotherhood, Mohammed Badie, anafungwa na alihukumiwa adhabu ya kifo.

Kwa mujibu wa wataalamu, vita vya uongozi vinafurukuta katika kundi hilo kati ya Mahmoud Ezzat, kiongozi wa walinzi wa zamani na Mohamed Kamal, kiongozi wa tawi la operesheni maalum.

Vitendo vya vurugu

Kamal alishutumiwa kupanga mashambulizi na ambayo yalimuua Mwanasheria Mkuu Hisham Barakat mwezi Juni 2015. Siku chache zilizopita, shambulizi jingine lilimlengagari Naibu Mwanasheria mkuu.

Kundi la Muslim Brotherhood pia linatuhumiwa kula njama dhidi ya uchumi wa Misri kwa kujihusisha na soko haramu la sarafu za kigeni ili kusababisha mfumko wa bei.