NIGERIA-USALAMA

Visa vya utekaji nyara vyakithiri kaskazini mwa Nigeria

Akari polisi wa Nigeria wakipiga doria katika jimbo la Bauchi.
Akari polisi wa Nigeria wakipiga doria katika jimbo la Bauchi. AFP

Watu kumi na moja, ikiwa ni pamoja na watoto watatu, walitekwa katika kijiji cha Tipchi, katika jimbo la Bauchi kaskazini mwa Nigeria. Mpaka sasa watu hao hawajaachiliwa, kwa mujibu wa chanzo cha polisi nchini Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Utekaji ulifanywa na watu wenye silaha siku ya Jumatatu katika kijiji hiki, kwenye umbali wa kilomita 120 kutoka mji mkuu wa jimbo Bauchi.

Watekaji nyara waliwapigia simu ndugu wa mateka na kudai malipo ya fidia kwa ajili ya kuachiliwa kwao.

Wanawake watatu, wasichana wanne na mvulana mmoja ni miongoni mwa watu waliotekwa nyara, kwa mujibu wa Ilya Muhammad, ambaye wazazi wake ni miongoni mwa mateka.

Amesema watu watatu walijeruhiwa walipokua wakitekwa nyara.

Kwa mujibu Sa'ad Abdullahi Abdulkadir, mmoja wa viongozi katika kijiji cha Tipchi, polisi na askari wametumwa katika eneo hilo kwa minajili ya kuwatafuta mateka.

Kijiji cha Tipchi kinapatikana katika misitu mkubwa, ambapo watu kadhaa walitekwa nyara hivi karibuni.