ZIMBABWE

Wanasiasa wakosoa uteuzi wa mkwe wa Mugabe kuwa CEO wa shirika lake la ndege

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe. REUTERS/Philimon Bulawayo

Siku chache baada ya bodi ya wakurugenzi ya shirika la ndege za Zimbabwe kumtuea, Simba Chikore ambaye ni mkwe wa rais Robert Mugabe, upinzani umekashifu uteuzi wake, huku hata hivyo ukioneshwa kutoshangazwa na hatua hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Chikora ambaye amemuoa mtoto pekee wa rais Mugabe, Bona Mugabe-Chikora, alitangazwa kuchukua nafasi hiyo mwanzoni mwa juma hili.

Uteuzi wake umekuja wakati huu utendaji wa shirika hilo ukikosolewa pakubwa, kutokana na kushindwa kujiendesha kwa faida kwa miaka kadhaa, huku ndege yake ikidaiwa kufanya kazi pale rais Mugabe anapotaka kusafiri.

Mwandishi wa idhaa ya RFI lugha ya kiingereza, Laura Bagnetto, amezungumza na aliyewahi kuwa waziri wa fedha wa nchi hiyo, Tendai Biti, ambaye amesema rais Mugabe anajali familia yake pekee na hana mapenzi na nchi hiyo.

Haya yanajiri wakati huu Serikali ikikabiliwa na hali mbaya ya kifedha ambapo imeshindwa kuwalipa mshahara kwa wakati wafanyakazi wake wa uma hali iliyosababisha maandamano.