DRC-ICGLR-SADC

Jumuiya ya ICGLR na SADC kuandaa mkutano wa pamoja kuhusu DRC

Nembo ya jumuiya ya nchi za maziwa makuu ICGLR
Nembo ya jumuiya ya nchi za maziwa makuu ICGLR http://m.portalangop.co.ao/angola/en

Kumeandaliwa Mkutano wa Viongozi wa Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR utakaofanyika Oktoba 26 mwaka huu mjini Luanda, Angola kwa lengo la kurejesha amani na maridhiano juu ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya maandamano ya Septemba 19.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu umeandaliwa na ICGLR kwa kushirikiana na jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC, utafanyika wakati hali ya kisiasa nchini DRC imesalia kuwa tete kutokana na mvutano unaoendelea kushuhudiwa kati ya Serikali na muungano wa upinzani.

Katika mahojiano na idhaa hii ya RFI waziri wa mambo ya nje wa Angola Georges Chikoti, amesema kuwa ni wazi uchaguzi hauwezi kufanyika katika muda uliopangwa kikatiba kama upinzani unavyodai, na kwamba inahitajika busara zaidi kuwahakikishia wanasiasa wanaoendelea kushikilia misimamo yao kuhusu swala hilo.

Chikoti amesema mkutano wa oktoba 26 mwaka huu, utatanguliwa na Mkutano wa wataalamu wa kimataifa kutoka umoja wa afrika, umoja wa mataifa UN, na wengine kutoka jumuia ya nchi za Ukanda wa maziwa makuu.

Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika, SADC, pamoja na wakuu wengine wa kimataifa wamekuwa wakikutana katika mikutano ya faragha, kutathmini kuhusu mustakabali wa taifa hilo, vyanzo vya kidiplomasia Vimesema.

Wakati haya yakiendelea nchi za magharibi zimeendelea kuweka shinikizo kwa Serikali ya rais Josephu Kabila kuondoka madarakani ifikapo mwezi December mwaka huu kama katiba inavyoelekeza.