NIGER-USALAMA

Niger: zaidi ya wanajeshi 20 wauawa katika kijiji cha Tazalit

Shambulizi la wanajihadi limefanyika katika kambi ya wakimbizi wa Mali mjini Tazalit katika mkoa wa Tahoua (picha ya kijiji cha Tahoua).
Shambulizi la wanajihadi limefanyika katika kambi ya wakimbizi wa Mali mjini Tazalit katika mkoa wa Tahoua (picha ya kijiji cha Tahoua). Eco Images / Universal Images Group

Jeshi la Nigeria limepata pigo kubwa kwa kuwapoteza askari wake 22 waliouawa Alhamisi wiki hii katika shambulio la wanajihadi katika kambi ya wakimbizi kutoka Mali katika kijiji cha Tazalit katika mkoa wa Tahoua. Shambulizi hili lilitokea mchana na limewashangaza wanajeshi.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni kwa mara ya kwanza kuwepo na idadi kubwa ya askari waliouawa katika eneo la kaskazini mwa mkoa wa mpakani wa Tahoua na kaskazini mwa Mali. Askari 22 waliuawa kwa kupigwa risasi kichwani.

Mapigano nchini Niger yamekuwa tishio katika ukanda huo wa Magharibi, askari walijeruhiwa katika shambulio hilo, maofisa wa eneo hilo wamesema yawezekana vifo vikaongezeka.

Kundi hilo la wahalifu liliwapiga risasi askari hao waliokua wakilinda kambi ya wakimbizi kutoka Mali mchana kweupe kwenye saa 8 saa za Mali. Tukio hilo lilitokea kilomita 35 magharibi mwa wilaya ya Tassara.

Baada ya kitendo hiki kiovu, wauaji hao walitimka wakielekea kwenye mpaka wa MAli, huku wakibeba silaha na vifaa vingine vya jeshi pamoja na gari ndogo ya kijeshi.

Vyanzo vya usalama vinabaini kwamba operesheni ya kuwasaka inaendelea; kikosi cha jeshi la Ufaransa kiliopo katika ukanda huo pia kimepewa taarifa.

Ukanda wa magharibi na kati wa taifa la Mali umekuwa hauko salama kwa kipindi cha miaka minne sasa tangu ufaransa ilipoingilia kati jitihada za kuwaondoa wapiganaji wa jihadi.