MALI-UJERUMANI-USHIRIKIANO

Angela Merkel ziarani Mali

Angela Merkel a admis que son gouvernement s'était insuffisamment préparé à l'accueil des réfugiés, ce lundi 19 septembre 2016.
Angela Merkel a admis que son gouvernement s'était insuffisamment préparé à l'accueil des réfugiés, ce lundi 19 septembre 2016. REUTERS/Fabrizio Bensch

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameanza ziara yake ya siku tatu barani Afrika ambapo Jumapili hii Oktoba 9 amezuru nchi ya Mali. Bii Merkel katika ziara hii anatazamiwa kuzuru nchi ya Niger na Ethiopia.

Matangazo ya kibiashara

Lengo la ziara yake ni kuimarisha ushirikiano wa Ujerumani na nchi hizi tatu ili kuzuia wimbi la wahamiaji wa Afrika wanaojaribu kuingia Ulaya.

Angela Merkel amesema kusaidia Afrika kuwa tulivu na imara itasidia utatuzi wa mgogoro wa wahamiaji.

Angela Merkel atatembelea kikosi cha askari wa Ujerumani wanaoshiriki katika mafunzo ya askari wa Mali na katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali.

Ujerumani inataka kutuma askari zaidi barani Afrika, hasa katika maeneo yanayolengwa na mashambulizi ya wanajihadi.

Hivi karibuni Angela Merkel alitangaza ujenzi wa kambi ya kijeshi nchini Niger.